Friday, April 11, 2014
Ni sheria gani inayosimamia mikataba ya ajira Tanzania?
Kwa ujumla Sheria ya Mikataba inasimamia aina zote za mikataba Tanzania. Lakini kwa mikataba mahususi kuna sheria mahususi inayosimamia mikataba hiyo. Kwa mfano Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi inaelezea mikataba ya ajira. Kwa maana hiyo ni sawa kusema Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Mikataba zote zinasimamia mikataba ya ajira.
Kuna aina ngapi za mikataba?
Kuna aina kuu tatu (3) za mikataba ambazo unaweza kuajiriwa nayo, nazo ni:
• Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa: Kama jina linavyojieleza, kwa aina hii ya mkataba kipindi cha ajira hakiainishwi. Mara nyingine huitwa mkataba wa kudumu.
• Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa: Hii ni aina ya mkataba ambao umetaja kipindi cha muda. Chini ya mkataba huu kama kipindi kilichotajwa kikimalizika basi mkataba utakua umefikia mwisho. Mkataba wa kipindi cha muda uliotajwa unaweza kua kwa kipindi cha mwezi, miezi mitatu, mwaka mmoja, miaka miwili nakadhalika.
• Mkataba wa kazi maalumu: Hii ni aina ya mkataba ambapo mtu huajiriwa kufanya kazi maalumu. Pindi kazi inapoisha na mkataba hufikia mwisho. Kwa mfano, mtu anaweza kuajiriwa kushusha kreti za soda kutoka kwenye gari na pindi kazi ile inapoisha na mkataba hufikia mwisho.
Kama mhasibu ama mtu wa fani nyingine naweza kuajiriwa kwa mkataba wa kipindi cha muda kilichotajwa?
Ndiyo, Kutokana na kifungu cha 14 (1) (b) mkataba wa kipindi cha muda kilichotajwa ni kwa kada za wataalamu na mameneja. Ijapokua suala hili bado linalalamikiwa mara kwa mara kwani hauwezi kuajiri mtu ambae sio mtaalamu katika misingi hii. Sheria inaeleza kwamba wanatakiwa waajiriwe chini ya mkataba wa kazi maalumu au mkataba wa kipindi cha muda kisichotajwa/mkataba wa kudumu.
Ni nini taarifa ya maelezo ya maandishi na inahusisha vitu gani?
Taarifa ya maelezo ya maandishi ni orodha ya taarifa kuhusu mfanyakazi ambayo lazima mwajiri ampatie mfanyakazi pindi mfanyakazi anapoanza kazi. Taarifa ya maelezo ya maandishi ni lazima iwe na taarifa zifuatazao kuhusu mfanyakazi:
• Jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi
• Mahali alipoajiriwa
• Kazi yake
• Tarehe ya kuanza
• Muundo na muda wa mkataba
• Kituo cha kazi
• Saa za kazi
• Ujira(mshahara), njia za ukukotoaji wake na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu; na
• Kitu kingine kilichotajwa
Kama maelezo yaliyoelezwa hapo juu yamekwisha elezwa katika mkataba ulioandikwa na kupewa mfanyakazi basi mwajiri hana haja ya kumpa mfanyakazi taarifa ya maelezo ya maandishi. Ni jukumu la mwajiri kuhakikisha kwamba maelezo yote au vipengele vya mkataba vinaelezwa katika hali inayoeleweka na mfanyakazi. Ni muhimu kuweka mkataba katika lugha inayoeleweka kirahisi na mfanyakazi, iwe Kiingereza ama Kiswahili.
Ninaweza kuajiriwa kwa mkataba wa maneno?
Mikataba ya maneno inaruhusiwa; ijapokuwa mfanyakazi ni lazima apewe taarifa ya maelezo ya maandishi inayoelezea vitu vilivyotajwa hapo juu. Hata hivyo haishauriwi kuingia mkataba wa maneno wa ajira kwasababu itakapotokea suala la taratibu za kisheria jukumu la kuthibitisha ama kukanusha sharti la ajira linalodaiwa litakua ni la mwajiri. Kama mwajiri atashindwa kutoa mkataba wa ajira au taarifa ya maelezo ya maandishi basi atashindwa kuthibitisha sharti lolote lilitojwa na mgogoro unaweza kuamuliwa dhidi yake. Hivyo ni muhimu kumpatia mfanyakazi mkataba wa maandishi au angalua taarifa ya maelezo ya maandishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Popular Posts
-
Ni sheria gani inayosimamia mikataba ya ajira Tanzania? Kwa ujumla Sheria ya Mikataba inasimamia aina zote za mikataba Tanzania. Lakini...
-
PADZ HOTEL MBEYA inawatangazia wakazi wa Mbeya nafasi za kazi mbali mbali kwa walio na diploma au Cheti. Kwa maelezo zaidi piga simu 077...
-
Meneja wa Kampuni ya New Position Co.Ltd, Juma Burah akizungumza jambo na waandishi wa habari(hawapo pichani) ofisini kwake. Ba...
-
MARAFIKI WA ELIMU MBEYA(MEM) has a wide range of VOLUNTEER OPPORTUNITIES available in working with children projects training children abou...
-
WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA NEW POSITION WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MKURUGENZI WA KAMPUNI JUMA BURRAH AKIWA OFISINI KWAKE
-
Share on facebook Share on twitter Share on email Share on print More Sharing Services 0 New Positions Company Lt...
-
A. TANGAZO LA NGAZI YA CHETI {TANGAZO LA STASHAHADA LIPO CHINI} JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI Sim...
-
Ni yapi mafao ya kusitisha ajira? Mafao ya kusitisha ajira ama kuachishwa kazi ni haki/stahili zote anazotakiwa apate mfanyakazi kutokan...
Recent Posts
Categories
- NAFASI ZA KAZI (9)
- KAZI (5)
- AJIRA (4)
- MATANGAZO (4)
- MBEYA (3)
- MAWAKALA WA AJIRA (1)
- MIKATABA YA KAZI (1)
- SHERIA ZA KAZI (1)
- TANZANIA (1)
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2014
(17)
-
▼
April
(17)
- No title
- NAFASI MPYA ZA KAZI
- NEW POSITION CO LTD WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA EZEE...
- OFISI YA WAKALA WA AJIRA NA KAZI SASA YAFUNGULIWA ...
- EZEEMONEY MACHINE
- AJIRA KIBAO MBEYA UWSA.: MWISHO 30/4/2014
- Office Manager at Fugro - Tanzania
- Nafasi mpya ya kazi kutoka serikalini
- NAFASI ZA KAZI TIGO TANZANIA - MFS Zonal Manager,...
- nafasi za mafunzo ya ualimu kwa mwaka wa masomo 20...
- Engineering Standards Specialist at Bulyanhulu Gol...
- Mikataba ya Ajira
- Mafao ya Kusitisha Ajira
- TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI PADZ HOTEL MBEYA
- NAFASI ZA KAZI ZA KUJITOLEA MBEYA
- NAFASI ZA KAZI TBS. MWISHO WA MAOMBI NI 22 APRIL
- MAWAKALA WA AJIRA NA KAZI WANAPATIKANA MBEYA, WENY...
-
▼
April
(17)
Text Widget
“Find out what you like doing best and get someone to pay you for doing it.” –Katherine Whitehorn
Sample text
Label
Social Icons
Blog Archive
About The Author
Followers
Find us on Facebook
MKURUNGEZI JUMA BULLAH

Ezee Money Mashine

ADIVERTISE HERE

Chat
Try Relay: the free SMS and picture text app for iPhone.
Visitors
Counter
www.ajiranakazimbeya.com cont..+255718470499
Pages
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment